DAVID LUIZ anakumbana na panga la kocha Jose Mourinho baada ya wachezaji wakubwa kumvuruga kwenye mchezo uliopita wa ligi kuu.
Nyota huyo wa Brazil ndiye aliyelaumiwa kwa kiasi kikubwa na wachezaji wenzake kwa namna alivyocheza mchezo huo dhidi ya Newcastle.
Mourinho ameamua kumpiga panga katika kikosi kitakachocheza dhidi ya Schalke kesho kwenye Champions league.
Luiz alikumbana na kitimoto kutoka kwa wenzake baada ya mchezo huo wakati Mourinho alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko St James baada ya kipigo cha mabao 2-0.
Mtu wa karibu na Mourinho usiku wa jana amethibitisha kuwa Mourinho ameanza kupoteza imani kwa Luiz,ingawa bado hajafikiria kama anaweza kumuuza wakati wa dirisha dogo mwezi January.
Beki wa kulia Branislav Ivanovic, ambaye amecheza mechi tatu za Champions League msimu huu naye huenda akapigwa benchi na nafasi yake ikachukuliwa na Cesar Azpilicueta.
Eden Hazard pia anaweza kupigwa benchi baada ya kutoonesha kiwango cha kuvutia.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.