Thursday, November 14, 2013

Schumacher achomoa kurudi kwenye Formula1

MJerumani Michael Schumacher ameichomolea ofa ya Lotus ya kumtaka kurejea tena kutoka kwenye kustaafu na kushiriki kwenye mbio mbili za mwisho kumalizia msimu wa Formula1.

Dereva huyo mwenye miaka 44,bingwa mara saba wa dunia amekataa ombi hilo la kuziba nafasi ya Kimi Raikkonen aliyeumia.

Nafasi ya Raikkonen sasa itazibwa na dereva mwenzake Finn Heikki Kovalainen.

Lotus wanatarajia kutangaza maamuzi hayo baadaye leo Alhamis huko Texas kuelekea kwenye mbio za Jumapili za United States Grand Prix.

Meneja wa Schumacher,Sabine Kehm amesema ni kweli walitaka dereva huyo mkongwe arudi kwakuwa wanadhani bado ni imara lakini tayari ameshatulia na maisha yake mapya.

Schumacher alistaafu 2006 baada ya muongo mmoja wa kuwa na Ferrari,lakini alirejea tena akiwa na kampuni ya Mercedes 2010 na akastaafu mwishoni mwa msimu uliopita ambako alichukuliwa Lewis Hamilton.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.