CHELSEA, Arsenal na Manchester City ziko tayari baada ya hatima ya mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani kuwa haieleweki kwenye klabu hiyo.
Ripoti kutoka Ufaransa zinasema Cavani hana furaha katika klabu hiyo na ataangalia kuondoka na kusaka klabu nyingine mwishoni mwa msimu.
Cavani hana furaha akichezeshwa kama mshambuliaji wa pili kwa Zlatan Ibrahimovic na tayari anataka kuzungumza na mshauri wake juu ya kuondoka huko Parc des Princes.
Cavani alisaini mkataba wa miaka mitano na PSG waliolipa paundu milioni 50 kumchomoa Napoli.
Wakati wa usajili uliopita Manchester City waliripotiwa kutumbukiza ofa ya paundi milioni 29 kwa mshambuliaji huyo huku Chelsea nao wakihusishwa kwa karibu.
Ripoti mpya zinasema licha ya klabu hizo kuwekeza kwenye ushambuliaji katika vikosi vyao lakini bado udenda unawadondoka kwa Cavani.
Arsenal nao wanatajwa wanaweza kutumbukia kwenye kuisaka saini ya Cavani ili kuimarisha ushambuliaji japo pia Bayern Munich, Borussia Dortmund, Real Madrid na Barcelona wanafuatilia kwa karibu kama mshambuliaji huyo atarudi sokoni.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.