Mashindano ya kombe la challenge 2013 yanatarajia kuzinduliwa Ijumaa.
Mtendaji mkuu wa kamati ya mashindano Gerald Chege amesema uzinduzi huo utaamabatana na kumtambulisha mdhamini wa mashindano ya mwaka huu pamoja na wadhamini wengine washiriki.
Anasema uzinduzi huo utatoa picha kwa mashabiki wa soka wategemee kitu gani wakati mashindano yatakapoanza.
Katibu mkuu wa Baraza la vyama na vilabu Africa mashariki na kati Cecafa Nicholas Musonye amesema viwanja vitakavyotumika ni vile vilivyopo Nairobi na Machakos kwa hatua ya awali.
Amesema pia miji itakayohusika katika hatua ya mtoano ni Kisumu, Mombasa na Mumias.
Nchi zilizothibitisha kushiriki ni Uganda, Tanzania, Rwanda, Somalia, Sudan, Zanzibar, Eritrea na Zambia wakati Burundi bado hawajathibitisha.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.