Friday, November 15, 2013

Lampard aapa kutetea nafasi yake kombe la dunia

Frank Lampard leo anaiongoza timu ya Taifa ya England kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Chile utakaochezwa kwenye uwanja wa Wembley huku akikiri kuwa anapigania nafasi yake kwenye kombe la dunia 2014 nchini Brazil.

Kiungo huyo wa Chelsea mwenye miaka 35 atakuwa anacheza mchezo wake wa 103 akiwa na timu ya taifa na atavaa kitambaa cha unahodha kutokana na kutokuwepo kwa nahodha Steven Gerrard ambaye ni majeruhi.

Lakini Lampard anafahamu kuwa ana kazi kubwa ya kufanya ili kuipata nafasi hiyo kutoka kwa kocha Roy Hodgson.
Frank Lampard facts
  • Born: 20 June 1978
  • Alianza kuchezea timu ya Taifa England  v Belgium October 1999
  • Alikosa Euro 2000 na Kombe la dunia 2002 lakini akawa sehemu ya kikosi Euro 2004 na 2008 ,kombe la dunia 2006 na 2010  
  • Goli la kwanza kuifungia England ni dhidi ya Croatia August 2003
  • Amekuwa mchezaji wa 8 kuichezea timu ya taifa ya England mechi 100 na alifunga goli hilo kwenye mchezo dhidi ya Ukraine September

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.