Wednesday, November 6, 2013

LIGI KUU : Tambwe aendelea kufukuzia kiatu cha dhahabu,Maguri amfukuzia


Mshike mshike wa ligi kuu soka ya Tanzania bara umeendelea tena leo kwa michezo minne ya kukamilisha mzunguko wa kwanza.

 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 mbele ya wauza mitumba wa Ilala uncolonized never say die Titi Munda Mtwale wa kuchwela watoto wa jiji Ashanti United Wanakinyamantula kama nyali.

Mabao ya Simba yaliwekwa wavuni na Ramadhan Singano Messi,Amis Tambwe aliyefikisha mabao 10 na kuendelea kuongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu huku mabao mengine mawili yakitupiwa wavuni na Betram Mwombeki.

Hadi muamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani anapuliza kipyenga kushiria dakika 90 zimemalizika huku Ashanti wakiwa pungufu baada ya mlinda mlango wao Amani Simba kulimwa kadi nyekundu, Simba wamechomoza na ushindi wa magoli 4-2.





Huko Chamazi Complex maafande wa JKT Ruvu walikuwa na kibarua kizito mbele ya wagosi wa kaya Coastal Union kutoka Tanga.

Kwenye mchezo huo maafande wa JKT Ruvu wamelitumia vyema dimba lao la nyumbani na kuwachapa Costal Union kwa bao 1-0.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi mchezo ambao umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.

Katika mchezo huo JUMA LUZIO aliifungia Mtibwa akifikisha bao lake la nane huku SHAABAN KISIGA MALONE naye akitumbukia wavuni.

Naye Elius Maguri akatupia wavuni mabao mawili kwa upande wa Ruvu shooting na kufikisha mabao 9 akiendelea kumfukuzia Amis Tambwe wa Simba anayeongoza na mabao 10.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.