Kocha Jose Mourinho amewashiwa taa za kijani kusaini mshambuliaji mpya wakati wa usajili wa dirisha dogo mwezi January ili kuendelea na changamoto ya kuusaka ubingwa.
Mourinho binafsi anachanganywa na mshambuliaji Fernando Torres aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni 50 na Samuel Eto'o kufunga goli moja katika ligi kuu ya England huku Demba Ba,mshambuliaji chaguo la tatu kutofunga bao mpaka sasa tokea alipofunga dhidi ya West Bromwich March 2.
Chelsea wapo pointi tano nyuma ya vinara Arsenal baada ya kukubgali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Newcastle,lakini Mourinho tayari ameamua kufanya mabadiliko kwenye safu ya ushambuliaji.
Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez anaonekana kufit kwenye mipango hiyo ya Chelsea na anaweza kucheza hata Champions league kwakuwa timu yake ya Liverpool haishiriki kwenye michuano hiyo lakini tatizo kwa mshambuliaji huyo timu yake ya Liverpool wameshasema hauzwi msimu huu.
Romelu Lukaku yeye amepelekwa kwa mkopo Everton mpaka mwishoni mwa msimu na hawezi kurudishwa kwenye usajili huo wa dirisha dogo.
Chelsea walimkosa MColombia Falcao ambaye akachagua kwenda Monaco ambako mpaka sasa kashatupia bao 10.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.