Thursday, November 21, 2013

Cavani,Suarez waichukua tiketi ya mwisho kombe la dunia 2014


Uruguay imekuwa taifa la mwisho kukata tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia 2014 zitakazopigwa nchini Brazil baada ya kutoka 0-0 na Jordan katika mchezo wa pili hatua ya mtoano.

Uruguay katika mchezo wa kwanza walipata ushindi wa mabao 5-0 na katika mchezo huo wa pili uliopigwa Montevideo Uruguay walitawala sehemu kubwa ya mchezo na walikaribia kufunga baada ya kichwa kilichopigwa na Diego Godin kugonga mlingoti.

Mshambuliaji Edinson Cavani anasema wana furaha kubwa kukata tiketi hiyo na akiweka wazi kuwa ilikuwa ni ngumu kuipata tiketi ya kwenda Brazil.

Nchi hiyo ya America Kusini ambao kwasasa wanakamata nafasi ya sita kwenye ubora wa viwango vya dunia walishinda taji hilo 1930 na 1950 na wakafika nusu fainali kwenye fainali zilizopigwa nchini Africa Kusini 2010.

Itakumbukwa July 16, 1950, Uruguay walichukua ubingwa baada ya kuichapa Brazil 2-1 kwenye fainali huko Rio de Janeiro uwanja wa Maracana ambao ndio utatumika kwenye mchezo wa fainali 2014.


Sasa hizi ndio timu rasmi za kombe la dunia 2014 Brazil

Africa: 
Algeria, Cameroon, Ghana, Ivory Coast, Nigeria
Asia:
Australia, Iran, Japan, South Korea
Europe: 
Belgium, Bosnia-Hercegovina, Croatia, England, France, Germany, Greece, Italy, Netherlands, Portugal, Russia, Switzerland, Spain
North & Central America & Caribbean:
Costa Rica, Honduras, Mexico, United States
South America:
Argentina, Brazil (hosts), Colombia, Ecuador, Chile, Uruguay

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.