Tuesday, November 12, 2013

Siasa za Misri zamponza aliyeipa ubingwa wa Africa Al Ahly atoswa kikosini kisa Morsi

Timu ya Al Ahly mabingwa wapya wa Africa wamemtosa kikosini mchezaji aliyewapa taji hilo kutokana na siasa za nchi hiyo baada ya kuonesha ishara ya kumuunga mkono Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi.

Al Ahly imesema mchezaji huyo Ahmed Abdul Zaher hatakwenda kwenye klabu bingwa ya dunia ya vilabu ya FIFA itakayofanyika mwezi ujao nchini Morocco baada ya kuonesha ishara ya vidole vinne inayotafsiriwa ni kama ya kumuunga mkono Morsi.

Mshambuliaji huyo alifanya ishara hiyo wakati akishangilia goli kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Orlando Pirates ya Africa Kusini.

Morsi Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia kwasasa anakabiliwa na mashtaka ya mauaji kwa waandamanaji wakati wa vurugu zilizotokea Cairo mwaka uliopita.

Baada ya kutupia wavuni bao la pili Abdul Zaher alisheherekea kwa ishara hiyo ya vidole vinne inayochukuliwa ni ishara ya kumuunga mkono Morsi ishara inayofahamika kama Rabaa.

Akizungumza kuhusu hilo Abdul Zaher anasema kweli alionesha ishara hiyo ya Rabaa,lakini anasema hakuwa na maana yoyote ya kisiasa wala hakuwa na maana ya kuunga mkono upande wowote kikubwa alikuwa anakumbuka vifo huko Rabaa,raia yeyote na hata Polisi.

Wakati huo huo Waziri wa michezo wa Misri Taher Abu Zeid amesema mchezaji huyo anapaswa kuadhibiwa na klabu yake pamoja na chama cha soka EFA.

Abdul Zaher ni mwanamichezo wa pili kuadhibiwa kwa kuonekana kumuunga mkono Morsi baada ya bingwa wa Kung fu Mohammed Youssef kufungiwa kujihusisha na mchezo huo ndani na nje ya nchi hiyo kwa muda wa miaka miwili baada ya kuonesha ishara kama hiyo.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.