Friday, November 22, 2013
Blatter aiaminia Morocco
Zikiwa zimesalia wiki chache kueleka kwenye fainali za klabu bingwa ya dunia ya vilabu zitakazopigwa nchini Morocco,Rais wa Fifa Sepp Blatter anaamini kuwa nchi hiyo ya Morocco wako tayari kuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Rais huyo wa Fifa alikuwa akizungumzia maandalizi ya mwisho pamoja na nchi na timu husika wanachokitarajia katika michuano hiyo ya 10.
Mabingwa wa Asia Guangzhou Evergrande,wenyeji Raja Casablanca,mabingwa wa Ulaya kupitia UEFA Bayern Munich,mabingwa wa Africa Al Ahly ya Misri kupitia CAF,mabingwa wa Oceania kupitia OFC Auckland City ya Newzealand,mabingwa wa CONCACAF Monterrey ya Mexico na mabingwa wa America Kusini Atletico Mineiro ya Brazil ndio watakaokuwa wakiwania taji hilo.
Blatter amesema Morocco wako tayari kuvikaribisha vilabu hivyo vikubwa na tayari Fifa imepitia kutazama kinachoendelea katika maandalizi hayo huku akisema ni sifa kubwa kwa Morocco na Africa kimataifa.
Amesema wana imani kubwa na kamati ya mashindano ambayo pia imeungwa mkono na serikali.
Ametaja viwanja vitakavyotumika kuwa ni Agadir na Marrakesh ambavyo vipo kwenye hali nzuri na anaona kuwa yatakuwa mashindano yenye mafanikio makubwa.
Itakumbukwa Morocco waliomba uwenyeji wa fainali za dunia 2010 ambazo ziliandaliwa na Africa Kusini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.