Tuesday, November 12, 2013

Djokovic aendelea kutesa ATP,avikwa taji la ubingwa wa dunia mbele ya Nadal

Novak Djokovic ameendelea kutesa katika mashindano ya dunia ya ATP baada ya kufanikiwa kulitetea akimshinda mchezaji anayeongoza kwa ubora duniani Rafael Nadal.

MSerbia huyo ambaye alipoteza mchezo wake aliokutana na Nadal mwezi uliopita amepata ushindi wa 6-3 6-4 huko O2 Arena London.

Djokovic, 26, sasa anafikisha michezo 22 kucheza bila kufungwa na sasa nguvu zake anazielekeza huko Belgrade,ambako timu ya Serbia inacheza na Czech Republic katika michuano ya Davis Cup Ijumaa.




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.