Wednesday, November 27, 2013

Ancelotti akiri kutaka "kuua"mchezaji


Boss wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti amekiri kuwa alitamani kumuua mmoja wa wachezaji huko Stamford Bridge.

MTALIANO huyo aliyeiongoza Chelsea kupata mataji mawili Ligi kuu na kombe la FA katika msimu wake wa kwanza huko Magharibi mwa London lakini akatimuliwa mwaka mmoja baadaye.
Lakini wakati Ancelotti anafurahia mahusiano mazuri na wachezaji wakati akiwa the Blues, AC Milan, Paris Saint-Germain na sasa Real Madrid,anakiri kuwa kuna mchezaji mmoja ambaye hakutaka kumtaja ambaye anasema ni tatizo kubwa Stamford Bridge.

Anasema hakuwahi kuwa na matatizo na wachezaji lakini yupo mmoja hakuonesha heshima na alijaribu kummaliza lakini haikuwezekana.
Ancelotti hakutaka kumtaja mchezaji huyo japo anasema aliwahi pia Didier Drogba kwa kuchelewa baada ya kufika dakika 30 kabla ya mechi kuanza na akamuweka benchi lakini anasema mahusiano yao yaliimarika.

Kipigo chaipa Chelsea tiketi ya kusonga mbele,yaendelea kuongoza kundi E

Licha ya kukutana na kipigo cha bao 1-0 kuitoka kwa FC Basel ya Uswis,wazee wa darajani Chelsea wamefuzu hatua ya mtoano ya Champions League.

Hata hivyo kipigo hicho kinawafanya Chelsea kuwa wateja wa FC Basel ambao katika mchezo wa kwanza walipata ushindi wa mabao 2-1 Stamford Bridge huku Mohamed Salah akiwa ni mchezaji aliyefanikiwa kufunga kwenye mechi zote hizo mbili.

Hatua ya Chelsea kufuzu inatokana na Schalke kutoka sare na Steaua Bucharest ya Romania na hivyo kuendelea kuongoza kundi E.


Group E

Pld GD Pts
Chelsea
             5
              8
              9
Schalke
             5
              1
              8
Basel
             5
             -2
              7
Steaua Bucharest
             5
             -7
              3

Tuesday, November 26, 2013

Uefa Champions League mzigoni

Ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi inaendelea leo kuisaka tiketi ya kuelekea kwenye hatua ya mtoano.

Arsenal waliokaa kwenye kundi la mtego watakuwa na kibarua cha kutaka kufanya vizuri ili kujiweka mguu sawa na hatua ya mtoano huku Chelsea nayo ikihitaji matokeo mazuri dhidi ya mbaya wao aliyewafunga kwenye mchezo wa kwanza.

FC Barcelona nao wako mzigoni kama ilivyo kwa Dortmund na Napoli na AC Milan pia dhidi ya Celtic


Mechi za leo

Monday, November 25, 2013

CHALLENGE CUP : Kilimanjaro Stars yaenda Nairobi na matumaini kibao


Timu ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars imeondoka kuelekea nchini Kenya kwa mashindano ya kombe la challenge linalotaraji kuanza kuunguruma November 27.


Kilimanjaro Starz imeondoka na matumaini kibhao ya kurejea na kikombe hicho kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

Wachezaji waliomo katika msafara huo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Hata hivyo, washambuliaji Samata na Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).

Kilimanjaro Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.

Pacquiao sasa kiu yake ni Floyd Mayweather

Manny Pacquiao sasa yupo tayari kupigana na Floyd Mayweather lakini anasema ni juu ya bondia huyo wa Marekani kuamua lini anataka pambano hilo.

Pacquiao, kutokea Philippines,hapo jana amepata ushindi wake wa kwanza baada ya miaka miwili  baada ya kumshinda Brandon Rios na kunyakuwa taji la WBO uzito wa welter.

Anasema kazi yake ni kupigana kwahiyo yupo tayari kupigana na Mayweather.


Mapambano 10 yaliyopita ya Manny Pacquiao

  • 23 Nov, 2013: v Brandon Rios (US), won (pts)
  • 8 Dec, 2012: v Juan Manuel Marquez (Mex), lost (KO 6th)
  • 9 Jun, 2012: v Timothy Bradley (US), lost (pts)
  • 12 Nov, 2011: v Juan Manuel Marquez (Mex), won (pts)
  • 7 May, 2011: v Shane Mosley (US), won (pts)
  • 13 Nov, 2010: v Antonio Margarito (Mex), won (pts)
  • 13 Mar, 2010: Joshua Clottey (Gha), won (pts)
  • 14 Nov, 2009: v Miguel Cotto (Pue), won (stoppage, 12th)
  • 2 May, 2009: v Ricky Hatton (GB), won (KO, 2nd)
  • 6 Dec, 2008: v Oscar de la Hoya (US), won (retired, 8th)

AVB : Spurs kupigwa sita aibu yetu wenyewe


Kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas amesema kikosi chake kinatakiwa kuona aibu kwa kipigo cha mabao 6-0 kutoka kwa Manchester City.

Spurs imekubali kipigo kikubwa kwa mara ya kwanza tokea ilipofungwa 7-1 na Newcastle December 1996.

Kipigo hicho cha jana kimewaacha Spurs kukalia katika nafasi ya tisa wakiwa na point inane nyuma ya wanaoongoza ligi Arsenal.

Villas-Boas amesema kipigo walichokipata ni kikubwa na ambacho wanatakiwa kuona aibu wao wenyewe kwa kukosa umakini na kuruhusu kipigo kikubwa ambacho hawakustahili.

Friday, November 22, 2013

Mourinho ambwatukia mkuu wa waamuzi

Boss wa Chelsea Jose Mourinho amemponda mkuu wa waamuzi Mike Riley kwa kuomba msamaha kwa West Brom kufuatia penati iliyotolewa dakika za mwisho kwenye mchezo wao dhidi ya Chelsea.

Mourinho anamini kitendo cha Riley kinaibua hatari kubwa huku akisema hakuna mtu aliyempigia simu kumuomba radhi kwa bao la pili la West Bromn ambalo mchezaji wa Chelsea Ramires alifanyiwa madhambi na Steven Reid lakini mwamuzi akaacha wakaenda kufunga.

Kocha huyo ameyasema hayo baada ya Riley kupiga simu kwa West Brom kuwaomba radhi kwa penati iliyotolewa na Andre Marriner dakika za lala salama iliyofanya matokeo kumalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.


Blatter aiaminia Morocco


Zikiwa zimesalia wiki chache kueleka kwenye fainali za klabu bingwa ya dunia ya vilabu zitakazopigwa nchini Morocco,Rais wa Fifa Sepp Blatter anaamini kuwa nchi hiyo ya Morocco wako tayari kuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Rais huyo wa Fifa alikuwa akizungumzia maandalizi ya mwisho pamoja na nchi na timu husika wanachokitarajia katika michuano hiyo ya 10.

Mabingwa wa Asia Guangzhou Evergrande,wenyeji Raja Casablanca,mabingwa wa Ulaya kupitia UEFA Bayern Munich,mabingwa wa Africa Al Ahly ya Misri kupitia CAF,mabingwa wa Oceania kupitia OFC Auckland City ya Newzealand,mabingwa wa CONCACAF Monterrey ya Mexico na mabingwa wa America Kusini Atletico Mineiro ya Brazil ndio watakaokuwa wakiwania taji hilo.

Blatter amesema Morocco wako tayari kuvikaribisha vilabu hivyo vikubwa na tayari Fifa imepitia kutazama kinachoendelea katika maandalizi hayo huku akisema ni sifa kubwa kwa Morocco na Africa kimataifa.

Amesema wana imani kubwa na kamati ya mashindano ambayo pia imeungwa mkono na serikali.

Ametaja viwanja vitakavyotumika kuwa ni Agadir na Marrakesh ambavyo vipo kwenye hali nzuri na anaona kuwa yatakuwa mashindano yenye mafanikio makubwa.

Itakumbukwa Morocco waliomba uwenyeji wa fainali za dunia 2010 ambazo ziliandaliwa na Africa Kusini.

Simunic alimwa faini kwa unazi



Beki wa Croatia Josip Simunic amepigwa faini ya dola 2,600 kwa ubaguzi baada ya kuwaongoza kwa kipaza sauti mashabiki kuimba nyimbo zilizokuwa zikitumiwa na utawala wa kinazi wakati wa vita ya pili ya dunia.

Simunic mwenye miaka 35 amepinga kuhusisha suala hilo na siasa wakati alipotumia kipaza sauti kuwaongoza kwa pamoja mashabiki kuimba baada ya kuifunga Iceland na kukata tiketi ya kucheza kwenye fainali za kombe la dunia.

Fifa bado wanafikiria kama wamchukulie hatua zaidi za kinidhamu yeye binafsi na wanasubiri ripoti ya waamuzi na pia ikikusanya taarifa kutoka kwa waangalizi wa kupinga ubaguzi kwenye soka barani Ulaya.

Thursday, November 21, 2013

Fifa yambeba Ronaldo tuzo ya Ballon d’Or


FIFA imetangaza kuongeza mwisho wa upigaji kura za kuwania tuzo ya Ballon d’Or 2013 mpaka November 29.

Maamuzi hayo huko Hispania yamechukuliwa ni kama ya kumbeba Cristiano Ronaldo dhyidi ya wapinzani wake kama Lionel Messi, Franck Ribery na Zlatan Ibrahimovic,baada ya nahodha huyo wa Ureno kupiga hat trick dhidi ya Sweden na kuipa tiketi timu yake ya Taifa kukata tiketi ya fainali za kombe la dunia 2014.

Mwisho wa makocha,manahodha na waandishi wanaopiga kura hizo kuwasilisha majina matatu ya juu ilikuwa November 15,saa kadhaa baada ya kumalizika kwa michezo ya hatua ya mtoano na Rebery anayecheza Bayern Munich alikuwa akipewa nafasi zaidi ya kuibuka na ushindi wa tuzo hiyo.

Na sasa tarehe imesogezwa mpaka Ijumaa ya November 29 na kura zinaweza kubadilika na kuelekea kwenye kiwango cha sasa kama alichokionesha Ronaldo hatua inayoonekana kumbeba zaidi mshambuliaji huyo anayepigiwa chapuo kuibuka na tuzo hiyo.

Chelsea,Man U zatiana pembe kumnasa kinda wa miaka 8


Chelsea na Manchester United wanatiana pembe kumuwania kinda wa miaka nane wa Argentina.

Real Madrid, Barcelona, Milan na Atletico Madrid pia zinafuatilia kwa karibu maendeleo yake akionekana ni kama Lionel Messi wa baadaye.

Kinda huyo Claudio Gabriel Nancufil,amepewa jina la utani la Snow Messi,na anachezea kwenye timu ya watoto ya Bariloche ya Argentina.

Nancufil anaelezewa kuwa ni mwenye uwezo mkubwa wa kukokota mpira na uwezo wa kumiliki mpira na kucheza nao akitumia mguu wa kushoto na pia ni mdogo kwa umri wake kuanza kufananishwa na Messi.

Familia yake tayari imempata wakala ambao ni Sueno Comunicaciones,kuzuia mpango wa kinda huyo kwenda Ulaya wakati vilabu vitano vikubwa vikihitaji huduma yake.