Tuesday, March 18, 2014

Villas-Boas ala shavu Zenit St Petersburg


Aliyekua Kocha wa Tottenham na Chelsea, Andre Villas-Boas amekubali kusaini mkataba wa miwili na klabu ya Zenit St Petersburg.

Kocha huyo mwenye miaka 36, aliyetimuliwa na Spurs mwezi Desemba atachukua nafasi ya Luciano Spalletti.

Taarifa ya klabu hiyo imesema Villas-Boas atatangazwa rasmi kuwa Kocha mkuu wa Timu hiyo Alhamis Machi 20.

Kibarua cha Spalletti kiliota nyasi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza hatua ya 16 bora ambapo ilichapwa mabao 4-2 na Borussia Dortmund.

Villas-Boas aliwahi kuwa msaidizi wa Jose Mourinho kabla ya kujiunga na Academica na baadaye FC Porto za Ureno.

Akiwa na FC Porto aliwapa taji la ligi,na ligi ya mabingwa katika msimu wake wa kwanza kabla ya kujiunga na Chelsea mwaka 2011, lakini akatimuliwa kazi mwezi March mwaka 2012 baada ya kushindwa kuifikisha timu hiyo kwenye viwango bora.

Tottenham wakampa mkataba wa kuifundisha timu hiyo July 2012 akiiongoza kumaliza nafasi ya tano kwenye ligi kuu katika msimu wake wa kwanza akiikosa kidogo nafasi ya kucheza champions league.

Spurs wakamuonesha mlango wa kutokea baada ya kuklubali kipigo kizito cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool.

Sasa amesaini kuifundisha Zenit,inayomilikiwa na kampuni ya gesi ya Gazprom na ni moja ya watumiaji wakubwa ya fedha kwenye usajili wao na tayari walifanya kufuru ya kuwasajili Mbrazil Hulk kutokea FC Porto na kiungo Axel Witsel kutokea Benfica kwa dau la jumla ya paundi milioni 64 September 2012.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.