Monday, March 17, 2014
Mashabiki wachoshwa na vipigo AC Milan
Kocha wa AC Milan Clarence Seedorf na baadhi ya wachezaji wake wamekutana na mashabiki wenye hasira kufuatia timu hiyo kuchapwa mabao 4-2 dhidi ya Pama.
Mario Balotelli na Kaka wanafikiriwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliokutana na mashabiki hao vyumbani uwanjani.
Inakadiriwa mashabiki wapatao 300 walikuwa wakisubiri nje ya geti kabla ya mchezo huo na kulalama wakati basi la timu hiyo lilipokuwa linaingia.
Pia wakaacha sehemu ya uwanja wa San Siro ikiwa tupu ikiwa ni mgomo kufuatia timu hiyo kuwa katika kiwango kibovu.
Mashabiki wa AC Milan wana hasira wakati huu ambao timu hiyo haifanyi vyema na sasa ikiwa katika nafasi ya 12 katika msimamo wa Serie A na tayari wamesukumwa nje ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kula kibano cha mabao 4-1 kutoka kwa Atletico Madrid.
Mchezji wa zamani wa kikosi hicho Mholanzi Clarence Seedorf amembadili Massimiliano Allegri aliyeoneshwa mlango wa kutokea mwezi January na tokea amechukua kikosi hicho amekumbana na vipigo vitatu mfululizo katika ligi ya Serie A.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.