Friday, March 21, 2014
UEFA CHAMPIONS LEAGUE DRAW : Ni hatari,..hofu,uoga watanda kila timu....Muda unaongea
Droo ya robo fainali ya ligi ya mabingwa inafanyika baadaye leo.
Timu nane zilizofanikiwa kukata tiketi ya kucheza haatua hiyo zinasubiri kumjua nani atakuwa mpinzani wake kwenye hatua hiyo.
Timu zilizokata tiketi ya hatua hiyo ni Manchester United na Chelsea kutoka England,mabingwa watetezi Bayern Munich na Borussia Dortmund kutoka Ujerumani,Barcelona,Real Madrid na Atletico Madrid kutoka Hispania na PSG kutoka nchini Ufaransa.
Timu zote zilizoingia kwenye hatua hiyo zinaonekana kuwa na ukali wake japo Dortmund na Manchester United ndizo zinaonekana vibonde kutokana na matokeo katika ligi zao za nyumbani lakini haliwezi kuondoa ukweli kuwa timu zote 8 ni balaa na itakuwa robo fainali yenye utamu wake.
Draw hiyo itafanyika saa 9 Alasiri na unaweza kuifuatilia kupitia supersport channel 203
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.