Mshambuliaji
wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo anaelezwa kuwa mwanasoka
tajiri zaidi duniani kwasasa kwa wale ambao bado wanacheza.
Mchezaji
huyo bora wa dunia amempiga chini nyota wa Argentina na Barcelona
Lionel Messi katika orodha hiyo ya wachezaji matajiri akikusanya kitita
cha paundi milioni 148.
Nyota aliyestaafu David Beckham
ndiye alikuwa kinara wa utajiri kwa mwaka jana 2013 lakini tokea
alipostaafu soka kwasasa hana kigezo cha kuingia kwenye orodha hiyo
inayoshirikisha wachezaji ambao bado wanacheza.
Messi
yupo kwenye nafasi ya pili akiwa anaingiza kiasi cha paundi milioni 146
akifuatiwa na Eto'o anayeingiza paundi milioni 85 wakati Wayne Rooney
yeye anaingiza paundi milioni 84 na Kaka
anakamilisha tano bora akikusanya kitita cha paundi milioni 82.
Orodha hiyo ni kwa mwaka husika na hauhusiani na miaka iliyopita.
Shuka na 10 bora ujionee.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.