Droo ya hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya imefanyika na kila mmoja kamjua mpinzani wake,huku mechi nyingine zikiwa za kulipa kisasi.
Manchester United imepangwa kucheza na Bayern Munich huku Chelsea ikipangwa kukutana na Paris St-Germain.
Mabingwa wa Hispania, Barcelona watapambana na Atletico Madrid, huku Real Madrid ikipangwa kukutana na Borussia Dortmund.
Mechi zao za mzunguko wa kwanza zitaanza April 1 na 2 marudiano ikiwa April 8 na 9.
Fainali ya michuano hiyo itapigwa huko Lisbon dimbam la Estadio da Luz Mei 24.
Manchester na Bayern wanakutana tena tokea walipokutana mwaka 1999 kwenye fainali ambapo Ole Gunnar Solkjaer na Teddy Sheringham waliiwezesha Manchester kutwaa kikombe chini ya Kocha wao Alex Ferguson.
Mara baada ya kupangwa kwa timu hizo nchini Switzerland, kiungo mshambuliaji wa Bayern, Philipp Lahm amesema kuwa hawawezi kubweteka na nafasi waliyonayo United kwa sasa katika ligi kuu na kusema kuwa watasafiri mpaka Manchester kwa kazi moja tu, nayo ni kufunga magoli.
Chelsea inayoongoza kwenye msimamo wa ligi itaifuata PSG nchini Ufaransa katika mzunguko wa kwanza.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.