Mshambulizi wa Manchester United Robin van Persie amesema kuwa yuko tayari kuongeza muda wa mkataba wake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini amekuwa akihusishwa na madai ya kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo kwa kuwa hana uhusiano mzuri na kocha wake David Moyes na kumekuwa na fununu kuwa huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu.
Lakini mchezaji huyo kutoka Uholanzi amesema kuwa anaridhika kucheza chini ya Moyes.
Amesema ana furaha ya kuwepo United,alisaini mkataba wa miaka minne na anapenda kuongeza muda wa mkataba kuendelea kuitumikia klabu hiyo iliyoyumba katika msimu huu.
Robin van Persie
- 15 Aug 2012: Alitua Manchester United akitokea Arsenal kwa dau la paundi milioni 24
- 2012-13: Alifunga mabao 26 katika mechi 38 za ligi kuu
- 2013-14: Amefunga mabao 10 katika mechi 16
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.