Monday, March 17, 2014
BAADA YA KADI NYEKUNDU : Mourinho akataa Foy kuwachezesha Chelsea
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema mwamuzi Chris Foy asiruhusiwe tena kuchezesha mechi za Chelsea baada ya kuwaonesha kadi nyekundu Willian na Ramires kwenye mchezo wao wa Jumamosi wakikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Aston Villa huku yeye mwenyewe akitolewa na mwamuzi huyo na kutakiwa kukaa jukwaani.
Mourinho amesema alijaribu kuzungumza na Foy baada ya mchezo huo lakini haikuwezekana akiongeza kuwa bodi ya waamuzi inatakiwa kuwa makini na kutazama kama mwamuzi huyo aendelee kuchezesha mechi za Chelsea.
Anasema hana uwezo wa kuomba hilo lakini wafikirie na kuona mwenendo wa mwamuzi huyo kila anapochezesha mechi za Chelsea ni lazima kunatokea tatizo na kadi nyekundu jambo ambalo hata wachezaji walilifahamu kabla na takribani wiki nzima walikuwa wakimzungumzia Foy kwa vitendo vyake dhidi ya klabu hiyo.
Foy rekodi yake inaonesha kuwa tayari amewatoa wachezaji sita wa Chelsea kwa kadi nyekundu katika michezo 8 na kwasasa mara mbili amewaonesha kadi nyekundu wachezaji wawili katika michezo miwili baada ya kuwatoa Jose Bosingwa na Didier Drogba kwenye mchezo dhidi ya Queens Park Rangers msimu wa 2011-12.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.