Tuesday, March 18, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE : Drogba arejea Stamford Bridge,asema hata akifunga hatashangilia


Ramires na Willian wako huru kucheza kwenye mchezo wa leo wa Champions league wakati Chelsea itakapokuwa wenyeji wa Galatasaray licha ya kutolewa kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Aston Villa Jumamosi.

Ashley Cole ana maumivu ya goti na hakufanya mazoezi ya hapo jana Jumatatu lakini David Luiz amejumuika na wenzake na anaweza kucheza nafasi ya Nemanja Matic kwenye kiungo cha kati kwakuwa mchezaji huyo haruhusiwi kucheza michuano hiyo kama ilivyo kwa Mohamed Salah ambaye tayari alicheza michuano hiyo akiwa na FC Basel.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba, 36, anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza kwa upande wa Galatasaray.
Boss wa Chelsea Jose Mourinho anaamini mkongwe Drogba bado ni mshambuliaji bora duniani.

Drogba aliyetimka Stamford Bridge June 2012 anarejea tena London huku mashabiki wa Chelsea wakimsubiri kumpa mapokezi makubwa.

Mourinho anasema hakuna anayejua kama Drogba yuko sawa na alivyokuwa na umri wa miaka 26 wakati huu ambapo ametimiza miaka 36 lakini bado kocha huyo anamuona kama mshambuliaji bora duniani.

Drogba mwenyewe anasema kama akifanikiwa kufunga goli kwenye mechi hiyo hatashangilia.

Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast ametupia wavuni mabao 157 katika mechi 342 alizoichezea Chelsea.


Didier Drogba's Chelsea record
  • Debut: v Manchester United, 15 August 2004
  • First goal: v Crystal Palace, 24 August 2004
  • Appearances: 342
  • Goals: 157
  • Honours: Premier League: 2004-05, 2005-06, 2009-10; FA Cup: 2006-07, 2008-09, 2009-10, 2011-12; League Cup: 2004-05, 2006-07 Champions League: 2011-12
  • Premier League top goalscorer: 2007, 2010

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.