Tuesday, March 25, 2014

Nadal,Serena Williams watesa Sony Open


Rafael Nadal amefanikiwa kutinga raundi ya nne ya michuano ya Sony Open baada ya ushindi wake wa 6-1 6-0 dhidi ya Denis Istomin wa Uzbekistan.

Ilimchukua mchezaji huyo namba moja kwa ubora wa dunia dakika 59 kujihakikishia nafasi yake ya kutinga hatua hiyo ya 16 bora akilisaka taji lake la kwanza la Miami.

Nadal, 27, anaungana kwenye hatua hiyo na bingwa wa Australian Open Stanislas Wawrinka, aliyemshinda Edouard Roger-Vasselin 7-5 6-4.

Wawrinka sasa atacheza na MUkraine Alexander Dolgopolov,aliyemshinda kwa 3-6 6-0 7-6 (7-5) dhidi ya MSerbian Dusan Lajovic.

Nadal atacheza na MTALIANO Fabio Fognini , aliyemshinda MSpain Roberto Bautista Agut 4-6 6-3 6-3.
Wakati huo huo bingwa mtetezi wa wanawake Serena Williams amekata tiketi ya kucheza robo fainali akimshinda Mmarekani mwenzake Coco Vandeweghe kwa 6-3 6-1 kwenye mchezo uliochukua dakika 79.

Williams, 32,sasa atacheza na MJERUMANI Angelique Kerber.

MRussia Maria Sharapova amefanikiwa kumshinda Kirsten Flipkens kwa 3-6 6-4 6-1 na sasa atacheza na bingwa wa zamani wa Wimbledon Petra Kvitov.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.