Friday, March 14, 2014

Mo Farah ndani ya London Marathon


Mwanariadha wa Uingereza, mzaliwa wa Somalia Mo Farah, amesema alifanya uamuzi bora kushiriki katika mashindano kadhaa ya barabarani kabla ya kushiriki katika mbio za London Marathon mwezi ujao.

Farah atakuwa miongoni mwa wanariadha watakaoshiriki katika mbio za kilomita ishirini na moja mjini New York Jumapili hii.

Mwanariadha mashuhuri wa Ethiopa, Haile Gebrselassie amesema ni mapema sana kwa Farah mwenye umri wa miaka 30 kushiriki katika mbio hizo za marathon, na badala yake kutoa ushauri kwake kutoa nafasi kwanza kwa mashindano ya uwanjani.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.