Monday, March 24, 2014

Baada ya Messi wa Simba kupasua kioo,uongozi wahaha kumaliza mambo,Logarusic asema ni ngumu kuukwepa mkono wa TFF


Uongozi wa Wekundu wa Msimbazi Simba unaendelea kutafakari kulimaliza suala la kinda wake nyota Ramadhan Singano Messi baada ya kuvunja kioo cha mlango wa vyumbani kwenye uwanja wa Taifa.

Singano nusura aingie mikononi mwa jeshi la Polisi baada ya tukio hilo lililofanyika baada ya mchezo kumalizika dhidi ya Coastal Union ambao Simba walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 lakini akaokolewa na kaimu katibu mkuu Ezekiel Kamwaga na kocha msaidizi Suleima Matola waliokwenda kuzungumza na askari waliofika kwa uwingi wao ili kumkamata mchezaji huyo.

Kinda huyo akiwa na hasira baada ya mchezo huo wakati wakiingia vyumbani alipofika kwenye mlango huo akaupiga teke kwa hasira na kioo kikavunjika.

Viongozi wa Simba wamekuwa wakihaha kulimaliza suala hilo ambalo hata hivyo linaonekana wanaweza kuliweka sawa kwa sehemu lakini hawataweza kuepuka kulipa faini na fidia ya uvunjifu wa kioo hicho cha mklango.

Kocha mkuu wa Simba Zdravko Rogarusic anasema hafahamu kuhusu tukio hilo lakini kama ikibainika kuwa mchezaji huyo amefanya tukio hilo uongozi hauwezi kuepuka adhabu kutoka TFF.

Hali ilivyokuwa baada ya  Messi wa Simba kuvunja kioo cha mlango
Mlango uliopasuliwa kioo na Messi
Askari wanataka kumkamata

 

Askari wakitoka kumfuata Messi





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.