Tuesday, March 18, 2014

Anelka kupigwa rungu lingine na FIFA kwa saluti ya nazi


Fifa wanafikiria kuongeza adhabu ya mshambuliaji aliyetimuliwa na West Bromwich Albion Nicolas Anelka baada ya maombi ya FA.

FA walimuadhibu Anelka kwa kumfungia mechi 5 baada ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 35 kushangilia kwa style isiyokubalika yenye ubaguzi ndani yake.

FA sasa imeomba kwa FIFA adhabu hiyo isiishie England peke yake na badala yake iwe duniani kote.

Maamuzi hayo ya FA inatokana na kutaka Anelka atumikie adhabu hiyo ipasavyo hata akiamia kwenye klabu nyingine yoyote.

Mwezi January Anelka aliadhibiwa kwa kushangilia goli lake dhidi ya West Ham United na alishangilia kwa style ya saluti za nazi ambazo haziruhusiwi japo mwenyewe alitetea kuwa haakuwa na maana yoyote ya kisiasa wala kibaguzi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.