Monday, March 31, 2014

Check Hamilton alivyotesa kwenye Malaysian GP


Lewis Hamilton ameshinda Malaysian GP akimuongoza mwenzake katika timu ya Mercedes Nico Rosberg.

Wawili hao wamezitawala nafasi mbili za juu huku Rosberg aliyemaliza nafasi ya pili akihakikisha dereva wa Red Bull Sebastian Vettel anakaa nyuma yake.



SONY OPEN : Djokovic amtesa Nadal

Mchezaji namba mbili kwa ubora duniani Novak Djokovic amemtesa mchezaji namba moja kwa ubora duniani katika tennis Rafael Nadal na kuchukua ubingwa wa Sony Open huko Miami.

Djokovic raia wa Serbia, 26,ameshinda kwa 6-3 6-3 na kunyakua kwa mara ya nne taji hilo na kumfanya kuwa juu ya Pete Sampras na mataji mawili nyuma ya Andre Agassi kwa wale waliochukua taji hilo mara nyingi zaidi.

Thursday, March 27, 2014

Real Madrid majanga tu

Timu ya Sevilla imeiweka njia panda Real Madrid kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kuwapa kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa jana usiku hiyo ikiwafanya Madrid kuumiza vichwa cha kufanya.

Sasa wamebaki na mlima wa kupanda kama wanataka kuupata ubingwa huku wakiomba mabaya kwa vinara Atletico Madrid ambao wana pointi 73 na Barcelona wanaokamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 72.

Mechi zilizobaki za Real Madrid

  • 29 March v Rayo Vallecano (h)
  • 5 April v Real Sociedad (a)
  • 12 April v Almeria (h)
  • 27 April v Osasuna (h)
  • 4 May v Valencia (h)
  • 7 May v Real Valladolid (a)
  • 11 May v Celta de Vigo (h)
  • 18 May v Espanyol (h)

Valdes kulikosa kombe la dunia

Golikipa wa Barcelona na Spain Victor Valdes atakosa fainali za kombe la dunia baada ya kuumia goti.

Kipa huyo alitolewa kwa machela mapema hapo jana kwenye mchezo ambao Barcelona ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Celta Vigo.

Barcelona wamethibitisha kuwa kipa huyo anahitaji upasuaji.

Valdes tayari ametangaza kuondoka kwenye klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu.


Wednesday, March 26, 2014

Inter Milan yamuweka kwenye rada Sagna

Inter Milan wanataka kumnasa beki wa Arsenal Bacary Sagna wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.

Wakali hao wa Italia wamekataa kuwa katika makubaliano na beki wa Manchester United Patrice Evra.

Rais wa Inter Milan Erick Thohir amesema wanataka kumsainisha Sagna kwakuwa wanataka kuweka uwiano wa timu kwakuwa kwasasa wana Yuto Nagatomo na Jonathan kama mmoja akiumia unahitaji mtu mwingine.

Moyes ajitwika zigo la lawama United


Boss wa Manchester United David Moyes amejitwika zigo la lawama kwa jahazi la timu hiyo kuzama ikiwa ni baada ya kipigo kingine kutoka kwa Manchester City.

Mabingwa hao watetezi wapo nafasi ya 7 ikiwa ni pointi 18 nyuma ya vinara Chelsea.

Moyes amesema yeye ndiye anachagua timu analazimika kubeba zigo la uwajibikaji japo inakatisha tamaa.


United dhidi ya Top five za Premier League
  • Chelsea: 0-0 draw (home); 3-1 defeat (away)
  • Man City: 4-1 defeat (away); 3-0 defeat (home)
  • Liverpool: 1-0 defeat (away); 3-0 defeat (home)
  • Arsenal: 1-0 win (home); 0-0 draw (away)
  • Everton: 1-0 defeat (home); away fixture 20 April

Bayern bingwa Bundesliga,waweka rekodi,Guardiola mkali wa mataji

Bayern Munich wamechukua taji lao la 24 la ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga huku wakiweka rekodi ya kuchukua ubingwa mapema zaidi baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hertha Berlin ikimfanya Pep Guardiola kuchukua taji akiwa na mechi 7 mkononi.

Ikiwa ni msimu wake wa kwanza, Guardiola sasa ameshinda mataji matatu katika miezi tisa Uefa Super Cup,Club World Cup na hilo la ligi.

Kiungo Toni Kroos alifunga bao la kwanza akimalizia kazi nzuri ya Thomas Muller kabla ya
Mario Gotze kutyupia la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya Bastian Schweinsteiger.

Franck Ribery akatupia la tatu huku Hertha Berlin bao la machozi likifungwa kwa penati na Adrian Ramos.

Ushindi huo unaifanya Bayeri kufikisha pointi 77 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.




Tuesday, March 25, 2014

Rais wa Al Ahly akamatwa kwa rushwa

Rais wa timu ya Al Ahly Hassan Hamdi amekamatwa na kusekwa ndani akikumbana na mashtaka ya rushwa.

Hamdi alikamatwa Jumapili na ataendelea kubakia rumande kwa siku 15 ili asiweze kutoroka Misri mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Hamdy amekataa madai yote anayohusishwa nayo.

Hassan Mahmoud Hamdi Ismail alizaliwa 1949 ni mwenyekiti wa 13 wa wakali hao wa Misri na mwenyekiti wa Al-Ahram advertising agency ambayo ni sehemu ya Al-Ahram Association .

Hamdi ambaye alicheza Al Ahly kama beki tokea mwaka 1969 mpaka 1978 alipata URais wa klabu hiyo mwaka 2002 baada ya mwenyekiti wa zamani Saleh Salim kufariki.

Nadal,Serena Williams watesa Sony Open


Rafael Nadal amefanikiwa kutinga raundi ya nne ya michuano ya Sony Open baada ya ushindi wake wa 6-1 6-0 dhidi ya Denis Istomin wa Uzbekistan.

Ilimchukua mchezaji huyo namba moja kwa ubora wa dunia dakika 59 kujihakikishia nafasi yake ya kutinga hatua hiyo ya 16 bora akilisaka taji lake la kwanza la Miami.

Nadal, 27, anaungana kwenye hatua hiyo na bingwa wa Australian Open Stanislas Wawrinka, aliyemshinda Edouard Roger-Vasselin 7-5 6-4.

Wawrinka sasa atacheza na MUkraine Alexander Dolgopolov,aliyemshinda kwa 3-6 6-0 7-6 (7-5) dhidi ya MSerbian Dusan Lajovic.

Nadal atacheza na MTALIANO Fabio Fognini , aliyemshinda MSpain Roberto Bautista Agut 4-6 6-3 6-3.
Wakati huo huo bingwa mtetezi wa wanawake Serena Williams amekata tiketi ya kucheza robo fainali akimshinda Mmarekani mwenzake Coco Vandeweghe kwa 6-3 6-1 kwenye mchezo uliochukua dakika 79.

Williams, 32,sasa atacheza na MJERUMANI Angelique Kerber.

MRussia Maria Sharapova amefanikiwa kumshinda Kirsten Flipkens kwa 3-6 6-4 6-1 na sasa atacheza na bingwa wa zamani wa Wimbledon Petra Kvitov.

KISA KESI YA MTOTO WAKE : Mahakama yamvua cheo Bosi wa Cricket India


Mahakama kuu nchini India imemtaka boss wa juu wa cricket kuachia nafasi yake ili kupisha uchunguzi wa haki katika madai ya upangaji matokeo kwenye ligi kuu ya India.

Jopo la majaji wawili limesema Rais wa bodi inayoendesha cricket nchini humo Narayanaswami Srinivasan amekuwa akichelewesha uchunguzi ambao unamuhusisha motto wake wakambo.

Mahakama hiyo imesema kama Srinivasan anayetajwa kama mmoja wa watawala wenye nguvu duniani kwenye mchezo huo hatajiuzulu katika nafasi yake hiyo wataamuru aondolewe.

Alichaguliwa kama mwenyekiti wa cricket duniani,baraza la kimataifa la cricket mwezi February na ataanza kazi hiyo mwezi July.

Mtoto wa kambo wa Srinivasan ,Gurunath Meiyappan, alihusishwa na upangaji wa matokeo mwezi uliopita.