Thursday, July 3, 2014

Hamoud alamba mkataba mnono Sofapaka

Kiungo aliyevunja mkataba wake na Simba Abdulhalim Hamoud Gaucho amemalizana na timu ya Sofapaka ya Kenya akisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo iliyopo kwenye ligi kuu ya Kenya.

Hamoud ambaye alikuwa na mkataba wa kuitumikia Simba,aliamua kuvunja mkataba wake mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuona mambo hayaendi anavyotaka huko Msimbazi.

Kiungo huyo amesema anamshukuru Mungu kwa kumalizana na Sofapaka kwa mkataba mzuri wenye maslahi makubwa kwake na sasa anajipanga kuitumikia timu hiyo na kuisaidia kutimiza malengo yake.

"Kaka namshukuru Mungu mkataba ni mzuri sana tena naona kama nimechelewa maana ni mkataba ambao mchezaji yeyote hawezi kuukataa,kwahiyo ninachofanya najipanga kuhakikisha siwaangushi na naamini nitaonyesha uwezo wangu na watu watakubali tu"alisema Hamoud.
 

Hamoud waweza kumuita Gaucho mbali na Simba amewahi kuzichezea Ashanti United,Azam FC na amewahi kucheza soka Uarabuni na ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes.

Blog ya Supermariotz tunamtakia kila la kheri,tunaamini anaweza na yeye ni mkali.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.