Tuesday, July 22, 2014
Dunga rasmi kocha mpya Brazil
Brazil wamemtangaza nyota wao wa zamani Dunga kuwa kocha mpya kwa mara ya pili.
Dunga alikuwa nahodha wa Brazil kwenye fainali za kombe la dunia 1994 wakishinda taji hilo na akaifundisha timu ya Taifa 2006 mpaka 2011.
Dunga amembadili Luiz Felipe Scolari,aliyeachana na timu hiyo baada ya Brazil kuishia nusu fainali kwenye kombe la dunia lililonmalizika hivi karibuni huku wakiacha kumbukumbu ya kupigwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani.
Kocha huyo aliwiongoza Brazil kwenye kombe la dunia 2010 nchini Africa Kusini na kuishia robo fainali.
Dunga anasema amefurahi kurudi tena kufundisha kikosi hicho cha Brazil.
Scolari, ameondoka pamoja na wasaidizi wake wote hiyo ina maana kuwa Dunga ataingia na utawala mpya.
Wakati huohuo kocha mkuu wa Argentina Alejandro Sabella, 59,ataamua hatima yake wiki ijayo baada ya kikosi chake kuchapwa bao 1-0 na Ujerumani katika mchezo wa fainali.
Wachezaji wanataka kocha huyo aendelee kubakia kwaajili ya fainali za Copa America 2015 zitakazopigwa Chile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.