Monday, July 14, 2014
Khedira anukia Arsenal
Arsenal wako karibu kuishinda Chelsea kuinasa saini ya kiungo wa Ujerumani Sami Khedira kutokea Real Madrid kwa dau la paundi la paundi milioni 23 ambalo tayari limekubalika.
Kwa mujibu wa ripoti hizo Khedira atasaini mkataba wa miaka minne licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa anatakiwa na Chelsea.
Mazungumzo ya muwakilishi wa kiungo huyo mwenye miaka 27 na Real Madrid yamevunjika na klabu hiyo imeamua kumuuza kuliko kuondoka bure baada ya mwisho wa msimu ujao.
Arsenal tayari imemnasa kwa dau la paundi milioni 30 mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez kutokea Barcelona,pia iko karibu kumnasa beki wa kulia wa Ufaransa Mathieu Debuchy kutokea Newcastle.
Boss wa Chelsea Jose Mourinho,ambaye alifanya kazi na Khedira wakati akiwa na Real anasaka kiungo mkabaji.
Khedira hakucheza kwenye mchezo wa fainali za kombe la dunia uliomalizika kwa Ujerumani kutawazwa mabingwa baada ya kuichapa Argentina kwa bao 1-0 liliwekwa wavuni na Mario Gotze.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.