WAZIRI mkuu wa zamani wa Italia ambaye ni mmiliki wa AC Milan Silvio Berlusconi ameshinda rufaa yake ya kudaiwa kumlipa msichana mwenye miaka chini ya 18 ili kufanya mapenzi.
Hukumu yake ya kwenda jela miaka 7 sasa imetupwa na jaji huko Milan katika kesi hiyo iliyopachikwa jina la Ruby.
El-Mahroug |
Mwaka uliopita mahakama ilimuona na hatia ya kulipa ngono kwa msichana mwenye miaka 17 dansa wa klabu ya usiku Karima El-Mahroug, anayefahamika kama Ruby, the Heart stealer.
Itakumbukwa Berlusconi amewahi kuhukumiwa kuitumikia jamii kwa kosa la kukwepa kodi.
Katika kesi hiyo ya Ruby wote wawili Berlusconi na El-Mahroug walikataa kuwa walifanya ngono.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.