Friday, July 4, 2014
Ronaldo amalizia machungu ya kombe la dunia kisiwani wakati mpenzi wake akitokelezea picha za utupu kwenye jarida
Cristiano Ronaldo ameyatupa kando maumivu ya kutokutolewa mapema kwenye fainali za kombe la dunia akionekana akiota jua huko Ugiriki kwenye kisiwa cha Mykonos wakati mpenzi wake Irina Shayk akipamba jarida kwa picha ya utupu.
Ronaldo alishindwa kuisaidia Ureno kusalia kwenye fainali za kombe la dunia na badala ya kuugulia maumivu ameamua kwenda kupumzika Ugiriki kabla ya kuanza msimu mpya.
Kwenye jarida la Maxim la July/August lililotoka linamuonesha mpenzi wa Ronaldo ambaye ni mwanamitindo Shayk, akitokea mbele ya jarida hilo akiwa mtupu.
Shayk ameliambia jarida hilo kuwa yeye na mpenzi wake Cristiano Ronaldo wanawapuuza wanaowachukia.
Anasema hajali kuhusu mawazo ya watu na hata Cristiano pia hajali hilo,kwakuwa kuna wengine wanakupenda na kuna wengine wanakuchukua,inabidi uwe imara.
Mbali ya kuwepa pozi la jarida hilo akiwa mtupu katika ukurasa wa mbele mrembo huyo pia ametokezea ndani ya jarida akiwa amepiga bikini.
Akizungumzia picha hizo Shayk anasema siku zote anapewa script ambazo zinamuonesha kwenye muonekana wa kichangudoa na kwake hafikiri kama zitamuweka kwenye upande mbaya wa kuonekana katika uhalisia wa kujiuza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.