Tuesday, July 22, 2014

Madrid yamalizana rasmi na Rodrigeuz


Real Madrid wamemalizana na mshindi wa kiatu cha dhahabu kwenye fainali za kombe la dunia James Rodriguez kutokea klabu ya Monaco ya Ufaransa.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Colombia amesaini mkataba wa miaka sita baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Inaelezwa kuwa mshambuliaji huyo amesajiliwa kwa dau la paundi milioni 63 na kumfanya kuwa mchezaji wa nne ghali duniani katika uhamisho akiwa nyuma ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez. 

Rodriguez alitupia wavuni mabao 6 katika mechi 5 za kombe la dunia nchini Brazil kikosi chake cha Colombia kiikiishia hatua ya robo fainali.

Uhamisho wake wa kuelekea Monaco uligahlimu paundi milioni 38 mwaka 2013,ikimfanya kuwa mchezaji wa pili ghali katika historia ya Colombia nyuma ya Radamel Falcao ambaye kwasasa katika historia ya nchi hiyo atakuwa anaongoza na Falcao akikaa nyuma yake.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.