Monday, July 14, 2014

Chelsea yaanza mazungumzo kumrudisha Drogba darajani


Chelsea wameanza mazungumzo ya kumrejesha mshambuliaji Didier Drogba huko Stamford Bridge.

Kocha Jose Mourinho anataka kumrejesha mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 kama mshambuliaji wa pili na pia atampa majukumu ya ukocha katika klabu hiyo.

Drogba ni nembo katika klabu hiyo ya Chelsea na Mourinho anaamini uwepo wake utasaidia hamasa katika msimu ujao.
Mourinho anahitaji mshambuliaji Zaidi kufuatia kuondoka kwa Samuel Eto'o wakati Demba Ba na Romelu Lukaku wanatarajiwa kuondoka hata kama itakuwa kwa mkopo huku Fernando Torres akitaka kuendelea kubaki licha ya kutakiwa na Inter Milan.

Drogba anawaniwa pia na klabu za huko Qatari ambazo zinataka kutoa dau nono la kufikia mpaka paundi milioni 3 kwa mwaka baada ya kukatwa kodi lakini mpango wa kurejea Chelsea ni kitu ambacho pande zote zinatamani ukamilike.
Mourinho ana mapenzi makubwa na Drogba na anaona anaweza kuleta changamoto kubwa katika kikosi hicho kilichobadilika kwa msimu ujao na inakumbukwa katika champions legue mwezi March wakati Chelsea ilipokutana na Galatasaray kocha huyo alikiri kuwa Drogba anaweza kurudi darajani.

Drogba akiwa na Chelsea alishinda mataji matatu ya ligi kuu,manne ya FA na Champions League na Mourinho anataka kuutumia uzoefu huo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.