Tuesday, July 22, 2014

Baada ya Gerrard kutema mzigo,Rooney kuchukua mikoba England



wayne rooney, steven gerrard, liverpool, manchester united, england, world cup, england captain, roy hodgson, mufc, man united, man utd, lfc,

WAYNE ROONEY anapewa nafasi kubwa Zaidi ya kuwa nahodha mpya wa timu ya Taifa ya England kufuatia kutundika daruga kwa Steven Gerrard kucheza mechi za kimataifa.

Gerrard alitangaza kujiweka pembeni kuitumikia timu ya taifa ambayo ameitumikia mara 114 na kuwa mmoja wa wachezaji walioitumikia timu ya taifa ya England mechi nyingi Zaidi.

Kuikacha kwake timu ya taifa sasa amemuachia mtihani kocha Roy Hodgson wa kusaka nahodha mpya huku Rooney akipewa nafasi kubwa Zaidi.

Nyota huyo wa Liverpool, 34,anasema kabla ya kufikia maamuzi yake alizungumza na mke wake Alex na nyota wa zamani wa England David Beckham na anasema amefanya maamuzi sahihi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.