Wednesday, July 16, 2014

Pellegrini aichomolea Brazil,ang'ang'ana na Man City


Wenyeji wa fainali za kombe la dunia 2014 Brazil wanasaka boss mpya baada ya kuachia ngazi kwa Luiz Felipe Scolari na kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini anatajwa kutakiwa.

Brazil ilipata kipigo kizito cha mabao 7-1 katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani kabla ya kupoteza kwa kuchapwa mabao 3-0 na Uholanzi katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu jambo liliwakera mashabiki wengi wan chi hiyo.

Karata yao inaelezwa kuwa wakaitupia kwa Pellegrini ambaye hata hivyo ameitosa kazi hiyo akitaka kuendelea kubakia huko Etihad.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.