Wednesday, July 23, 2014

Mzozo wa Ukraine waikimbiza Shaktar Donetsk


Shakhtar Donetsk watacheza mechi zake za nyumbani huko Magharibi katika mji wa Lviv uliopo zaidi ya maili 600 kwasababu ya mgogoro uliopo Ukraine.

Wachezaji sita wa kigeni wamegoma kurudi huko Donetsk wakihofia mzozo huo.

Wachezaji waliogoma kurudi baada ya mechi yao ya kirafiki huko Lyon ni wachezaji watano raia wa Brazil na mmoja kutoka Argentina ambao ni Alex Teixeira, Fred, Dentinho, Douglas Costa, Facundo Ferreyra na Ismaily.
Kikosi hicho sasa kitakuwa kina fanya mazoezi yake huko Kiev na kusafiri kwenda kucheza mechi zake za champions league na mechi za ligi huko Lviv.

Mapigano yanaendelea katika baadhi ya maeneo huko Donetsk.

Rais wa klabu hiyo Rinat Akhmetov amesema wachezaji hao wanautumia mgogoro huo kutaka kuhama na kwenda kucheza timu nyingine.

Shakhtar hapo jana wameifunga Dynamo Kiev 2-0 huko Lviv,katika mchezo wa ufunguzi wa msimu.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.