Tuesday, July 15, 2014

Cavani azitega Man U na Chelsea


MSHAMBULIAJI Edinson Cavani amemuagiza wakala wake kuchunguza timu ambayo anaweza kwenda katika ligi kuu ya England.

Cavani mwenye miaka 27 alijiunga Paris Saint-Germain akitokea Napoli kwa dau la paundi milioni 55 na alisaini mkataba wa miaka mitano lakini sasa anaonekana kutaka kuondoka.

Habari hiyo inaweza kuwa njema kwa Chelsea na Manchester United,ambao wote walihusishwa kuitaka huduma yake.
Cavani alipata mafanikio katika msimu wake wa kwanzaa na PSG, baada ya kuchukua ubingwa wa Ufaransa huku pia wakichukua kombe la ligi na cavani akitupia kambani katika mechi zote mbili.

Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ameripotiwa kutokuwa na furaha PSG kutokana na uwepo wa Zlatan Ibrahimovic ambao unamfanya acheze akitokea pembeni.
Akiwa Italia katika msimu wa 2012/13 alimaliza kama mfungaji bora wa Serie A.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.