Friday, July 18, 2014

Balotelli na mpenzi wake wamuita Wenger mezani


Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Mario Balotelli, 23,ameonesha nia ya dhati ya kutaka kujiunga na Arsenal baada ya kupiga picha mbele ya nembo za timu hiyo.

The Gunners walihusishwa kuitaka huduma ya mshambuliaji huyo kabla ya fainali za kombe la dunia mpango ambao ulififia.

AC Milan wako tayari kumuuza na pozi aliloweka ni kama anamwambia kocha wa Arsenal Arsene Wenger njoo unisajili.

Mpenzi wa Balotelli Fanny Neguesha ametupia picha hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram huku picha hiyo ikisindikizwa na neon PUMA ambao ni wadhamini wa jezi kwa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.