Ujerumani imefanikiwa kupanda katika viwango vya ubora dunia mpaka nafasi ya kwanza baada ya miaka 20.
Ushindi wao katika fainali za kombe la dunia umewapaisha kwa nafasi moja kutoka nafasi ya pili na sasa wamekaa kwenye nafasi ya kwanza na kuvunja utawala wa Hispania ambao wametupwa nafasi ya nane.
Arjentina wamekaa nafasi ya pili wakipanda kwa nafasi tatu huku Uholanzi wakipanda kwa nafasi 12 mpaka nafasi ya tatu.
Kwa barani Africa Algeria wamepanda nafasi ya kwanza wakifuatiwa na Ivory Coast na Nigeria wamekamata nafasi ya tatu huku Misri wajkikaa nafasi ya nne na Ghana nafasi ya tano.
Tanzania ipo nafasi ya 29 lakini kwa dunia wakikamatana nafasi ya 106 wakipanda nafasi 7 baada ya kujikusanyia pointi 287.
Shuka nayo na nafasi walizopanda zipo kwenye mabano.
1. Germany (+1)
2. Argentina (+3)
3. Netherlands (+12)
4. Colombia (+4)
5. Belgium (+6)
6. Uruguay (+1)
7. Brazil (-4)
8. Spain (-7)
9. Switzerland (-3)
10. France (+7)
11. Portugal (-7)
12. Chile (+2)
13. Greece (-1)
14. Italy (-5)
15. USA (-2)
16. Costa Rica (+12)
17. Croatia (+1)
18. Mexico (+2)
19. Bosnia and Hercegovina (+2)
20. England (-10)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.