Tuesday, July 22, 2014

Torres aingia kwenye rada za Atletico Madrid


Ripoti kutoka England zinadai kuwa Chelsea the Blues wako radhi kumuachia mshambuliaji wake mwenye miaka 30 Fernando Torres kuondoka katika klabu hiyo huku klabu yake ya zamani Atletico Madrid wakionesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Mtendaji mkuu wa Atletico Miguel Angel Gil Marin alikuwa jijini London wikiendi iliyopita kujadiliana kuhusiana na uwezekano wa mpango huo.

Katika mpango huo Atletico wapo tayari kutoa dau la paundi milioni 13 kwa Chelsea ili kuipata huduma ya Torres,na inaonekana the Blues wako tayari kukubaliana na mpango huo.

Torres alianza maisha yake ya soka kwenye klabu hiyo ya Atletico akifunga mabao 91 kwenye mechi 244 alizocheza kabla ya kuondoka huko Vincente Calderon mwaka 2007 na kujiunga na Liverpool.

Aliitumikia Liverpool kwa miaka minne ambako alifunga mabao 65 katika mechi 102 kabla ya kuhjiunga na Chelsea mwaka 2011 kwa dau la paundi milioni 50 na katika mechi 174 alizoichezea klabu hiyo amefunga mabao 45.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.