Wednesday, July 16, 2014
Chelsea yamalizana na Luis ikiendelea kuibomoa Atletico
Chelsea wamefikia makubaliano na mabingwa wa Hispania Atletico Madrid kumsainisha beki wa kushoto raia wa Brazil Filipe Luis.
Beki huyo mwenye miaka 28 kwasasa anafanya makubaliano ya maslahi binafsi na amefanya vipimo vya afya.
Msimu uliopita Luis alicheza katika mechi 44 akiwa na Atletico iliyoshinda taji la La liga kwa mara ya kwanza tokea 1996 na katika msimum huo pia walifika fainali ya Champions League.
Luis anaonekana kuwa mbadala wa beki Ashley Cole ambaye hakuongezwa mkataba na amekwishatimkia As Roma ya italia.
Atletico wamesema beki huyo wa zamani wa Deportivo La Coruna aliwambia kuwa anataka kuondoka na kujiunga na Chelsea inapofika mwisho wa msimu.
Anakuwa mchezaji wa pili kutokea Atletico kujiunga na Chelsea katika usajili unaoendelea wa majira ya joto baada ya mshambuliaji Diego Costa naye kusajiliwa kwa dau la paundi milioni 32.
Luis amecheza mechi 180 tokea alipotua Atletico akitokea Deportivo mwaka 2010.
Ameitwa mara nne kwenye timu ya taifa ya Brazil huku pia katika fainali zilizomalizika huko Brazil aliwekwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wangeweza kumbadili mtu wakati wowote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.