Monday, July 21, 2014

Drogba atuma salamu za kurudi Chelsea


Didier Drogba yupo karibu kurudi Chelsea kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mazungumzo yanaendelea huku Drogba akiwa tayari amewatumia ujumbe wachezaji wenzake wa zamani wa Chelsea kuwaelezea kuhusu kurejea kwenye klabu hiyo.

Chelsea wanaamini kuwa mchango wa Drogba utawasaidia ndani na nje ya uwanja.

Uzoefu wake na kushinda mataji kunaweza kuwasukuma wachezaji wengine kufanya kweli.

Kutua kwa Drogba kutaongeza nguvu safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo tayari wana Fernando Torres,wamemuongeza Diego Costa huku ikiwaruhusu kuondoka Demba Ba aliyetimkia Besiktas na Samuel Etoo aliyemaliza mkataba wake huku Lukaku akiwa bado haieleweki kama ataendelea kubaki kwenye klabu hiyo au atapelekwa kwa mkopo klabu nyingine.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.