Thursday, July 17, 2014
Mikel Obi mguu pande Chelsea
Chelsea wanajiandaa kumuuza kiungo wake MNigeria John Mikel Obi, 27,wakiwa katika mipango ya kuinasa saini ya kiungo wa Real Madrid Sami Khedira, 27,ambaye pia anatakiwa na Arsenal.
Kocha wa The Blues Jose Mourinho anataka kuongeza kiungo mwingine kikosini kabla ya kuanza msimu huku pia mpango wa kumnasa kinda Paul Pogba mwenye thamani ya paundi milioni 60 ukiingia shakani na sasa anamgeukia Khedira kwa paundi milioni 20.
Chelsea kuna kugombea namba katika sehemu ya kati ikimjumjumuisha nyota wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas lakini Mikel ndiye anayeonekana kukosa nafasi na anaweza kuondoka.
Mikel kaanza kikosi cha kwanza katika mechi 11 msimu uliopita na ripoti zinasema kuwa kuna timu za Italia katika Serie A zinamtaka ikiwemo Inter Milan na Thamani yake inaelezwa kuwa paundi milioni 10.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.