Monday, July 21, 2014
Serena ajianika na bikini
Mcheza Tennis Serena Williams alilazimika kujiondoa kwenye mashindano ya Wimbledon baada ya kuugua lakini nyota huyo wa tennis anaonekana sasa amepona baada ya kunaswa akiwa anajirusha na marafiki zake.
Mwanadada huyo mwenye miaka 32 alilazimika kujiondoa katika michuano hiyo ya Wimbledon mchezo wa wawili wawili akicheza na mdogo wake Venus dhidi ya Kritina Barrois na Stefanie Voegele.
Serena kwasasa hali yake inaonekana kuwa sawa baada ya kunaswa huko Pula, Croatia akiajiachia akiwa amepiga bikini.
Lakini pia akaonekana mitaa ya Michigan akiwa anakatiza mitaa huku akiwa ametupia kivazi kilichomchora mwili wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.