Monday, June 30, 2014

Suarez amuangukia Chiellin,aendelea kujikanyaga kwenye utetezi wake

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez amemuomba radhi mchezaji wa Italia aliyemng'ata Giorgio Chiellini na kusababishwa kupigwa adhabu ya kufungiwa mechi tisa za kimataifa na kifungo cha miezi minne kutojihusisha kwa namna yoyote na mchezo wa soka.

Suarez mwenye miaka 27 amesema ukweli ni kuwa Chiellini alipata maumivu ya kung'atwa baada ya kugongana.

Kauli hiyo inaendelea kujichanganya baada ya awali kusema kuwa alikosa balance na hakumng'ata Chiellini.

Hii ni mara ya tatu kwa Suarez kuhusika na tukio la kung'ata,itakumbukwa aliwahi kumng'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic April 2013 akiwa kwenye timu yake ya Liverpool na pia amewahi kumng'ata Otman Bakkal wakati alipokuwa akiitumikia Ajax mwaka 2010.

Suarez anajutia kitendo hicho alichomfanyia Chiellini na kuomba radhi kwa mchezaji huyo na familia ya mpira na kuahidi kuwa hatarudia tena kufanya kitendo kama hicho.

Chiellini mwenyewe amemtumia ujumbe Suarez kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, akimwambia yote yamesamehewa na anaamini FIFA watampunguzia adhabu.

Suarez atakosa mechi 9 za kwanza za ligi kuu ya England na anarejea katika soka October 26.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.