Thursday, June 19, 2014

Kocha Cameroon akerwa na kichwa cha Ekotto kwa Moukandjo


Cameroon wamesukumwa nje ya fainali za kombela dunia lakini tukio ambalo litakumbukwa kwenye mchezo wao dhidi ya Croatia waliokubali kipigo cha mabao 4-0 ni ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe kati ya Benoit Assou-Ekotto aliyempiga kichwa mchezaji mwenzake Benjamin Moukandjo.

Wawili hao walianza kubishana katika eneo lao kabla ya Ekotto kumchapa kichwa mshambuliaji huyo.

Kocha wa camerron Volker Finke anasema ameona tukio hilo na anataka kufuatilia kujua nini hasa kimetokea na kwanini wawili hao wamegombana.

Ugomvi huo uliendelea mpaka sehemu ya kuelekea vyumbani lakini mshambuliaji majeruhi Samuel Eto'o akaingilia kati na kuwatengenisha wachezaji hao.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.