Monday, June 30, 2014

Rais Mujica wa Uruguay aitusi FIFA kisa Suarez


Rais wa Uruguay Jose Mujica amewatukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita ''kundi la watoto wa Mbwa''.

Hatua hiyo inafuatia maafisa wa shirikisho hilo kumshushia rungu Luis Suarez akifungiwa mechi tisa za kimataifa na kupigwa marufuku kujihusisha na mchezo wa soka kwa miezi minne baada ya kupatikana na hatia ya kumng’ata mchezaji wa Italia Georgio Chiellin.

Rais huyo wa Uruguay anayesifika kwa kutotafuna maneno na kutumia matamshi makali ameiita adhabu hiyo kama adhabu ya kinazi.

Aliyatoa matamshi hayo kupitia televishini ya taifa alipokuwa anawapokea wachezaji wa timu hiyo baada ya kusukumwa nje ya fainali za kombe la dunia.

Rais huyo alifunika mdomo wake kwa mshutuko wa kile alichosema , lakini waandishi wa habari tayari walikuwa wamemrekodi.

Rais Mujica amesema FIFA ilimuadhibu Suarez kwa sababu ya maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa ya unyonge na akaitaja adhabu hiyo kama aibu kubwa kwa historia ya FIFA.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.