Monday, June 30, 2014
UDANGANYIFU : Roben akiri kujiangusha kudai penati
Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya na kujirusha ili timu yake ipate penalti japo anakiri hakufanyiwa madhambi na nahodha wa Mexico Rafael Marquez.
Roben ameomba radhi mashabiki kwa kudanganya na kujiangusha,akikiri wazi kuwa ilikuwa njia ya kutaka kuisaidia timu yake.
Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemponda mwamuzi wa mechi yao na Uholanzi Pedro Proenca kwa kuipendelea Uholanzi .
Herrera amesema kuwa Penalti hiyo ya dakika tatu kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo haikupaswa kutolewa na hiyo akiiona ni njama ya FIFA kuiondoa Mexico kwenye fainali hizo.
Herrera amesema haikuwa sahihi kwa mwamuzi kutoka Ulaya kuchezesha mchezo kati ya timu kutoka Ulaya dhidi ya timu kutoka Marekani ya kusini.
Anauliza kwanini FIFA hawakupanga mwamuzi kutoka Africa,Asia au kutoka Marekani Kusini.
Robben alikuwa akiingia kwenye lango la Mexico na kujiangusha kumdanganya mwamuzi na kusababisha penati ambayo ilitumbukizwa na Jan-Klaas Huntelaar iliyoipa tiketi ya kutinga robo fainali timu yake ya Uholanzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.