Wednesday, June 18, 2014

Mandzukic kuiongoza Croatia kwa cameroon


Kiungo Luka Modric na Mario Mandzukic wataiongoza Croatia kufufua matumaini ya kutinga kwenye hatua ya 16 bora wakati wanashuka kuikabili Cameroon.

Kikosi hicho chini ya kocha Niko Kovac kina matumaini makubwa kwa mchezo huo wa leo ambao unaweza kuwapa picha ya muelekeo wao kwenye fainali hizo.

Modric amepona maumivu ya mguu aliyoyapata kwenye mchezo wa ufunguzi ambao walichapwa mabao 3-1 na wenyeji Brazil katika mchezo wa kundi A.

Mandzukic anacheza mchezo wake wa kwanza wa fainali za mwaka huu baada ya kutumikia adhabu ya kutocheza mchezo mmoja baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa pili wa kuisaka timeti ya kutinga kwenye fainali hizo dhidi ya Iceland.

Kocha Kovac amesema Mandzukic ataongoza safu ya ushambuliaji na Modric yuko fit kwa asilimia 100 katika mchezo huo muhimu kwa pande zote mbili.

Kovac anasema watafanya lolote linalowezekana kuchukua pointi zote tatu japo akisema kutokuwepo kwa Samuel Etoo haiwapi unafuu kwakuwa kocha wa Cameroon Volker Finke anaweza kuwa na mpango B wa kuziba nafasi hiyo.

Cameroon walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mexico kwa kuchapwa 1-0.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.