Paris Saint-Germain wako tayari kutoa dau la paundi milioni 61 ili kumnasa Eden Hazard kutokea Chelsea.
Mabingwa hao awa Ufaransa wamelimwa faini ya paundi milioni 49 kwa kuvunja kanuni ya matumizi ya fedha ya kiungwana mwezi mmoja uliopita tayari wameilipa Chelsea paundi milioni 50 kuinasa saini ya beki David Luiz.
Pia wameonesha nia ya kuwataka Branislav Ivanovic, Oscar na Petr Cech lakini Hazard ndiye hasa wanamuhitaji na wanaamini Chelsea watamuuza.
Muwakilishi wa Hazard amekutana na mmiliki wa PSG Sheik Tamim bin Hamad al-Thani,na wako tayari kumpa ofa Hazard ya kulipwa paundi 230,000 kwa wiki.
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho anatarajia kukamilisha mpango wa kumalizana na mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa kabla ya fainali za kombe la dunia huku pia akiwataka Tiago, Filipe Luis, Koke na Diego Godin wote wa Atletico.
Tayari Costa mwenye thamani ya paundi milioni 32 amefuzu vipimo vya afya na sasa anakamilisha mjadala wa maslahi binafsi.
Pia mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas yanaendelea huku pia wang’amua vipaji wakiendelea kumfuatilia kiungo kinda mwenye miaka 19 Carlos Gruezo,anayechezea Stuttgart.
Wakati PSG wakimtolea macho Hazard tayari Chelsea imetangaza kumpatia jezi namba 10 atakayotumia kuanzia msimu ujao.
Jezi hiyo alikuwa akiitaka Hazard kwakuwa anasema tokea mdogo alipenda namba hyiyo kwasababu ilikuwa ikivaliwa na shujaa wake Zinedine Zidane.
Tayari amesema kuwa bado ana furaha ya kuendelea kubakia Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.