Friday, June 13, 2014

AIBU : Kocha Croatia ambwatukia muamuzi,asema ni bora warudi nyumbani kucheza Basketball

Kocha wa Croatia Niko Kovac ameibua malalamiko kwa muamuzi Yuichi Nishimura baada ya timu yake kula kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Brazil kwenye mchezo wa ufunguzi kombe la dunia.

Kovac amekuja juu baada ya Neymar kutooneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko Luka Modric katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo na baadaye wenyeji wakapewa penati nyepesi wakati Fred alipofanyiwa madhambi na Dejan Lovren.

Wachezaji wa Croatia hata walipomlalamikia muamuzi waliishia kupewa kadi za njano.
Katika mchezo huo pia kocha huyo analalamika kukataliwa kwa goli lao ambapo muamuzi huyo kutoka Japan alilikataa kwasababu Ivica Olic alimtendea madhambi Golikipa wa Brazil Julio Cesar wakati wakiwa hewani kugombea mpira.

Kovac anasisitiza kuwa haikuwa penati halali na anasema kwa maamuzi hayo ni bora wacheze mpira wa kikapu kwasababu ni maamuzi ya aibu.

Ameongeza kuwa kwao wanaona wamekosewa heshima na anasema kama huo ndio mwanzo wa kombe la dunia huko Brazil ni vyema wakarudi nyumbani kuliko kucheza fainali hizo.

Tazama hatua kwa hatua Neymar akimchapa Modric kiwiko na akaishia kupewa kadi ya njano na muamuzi.
 
 





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.